Header Ads

Ramaphosa azindua kampeni ya chama cha ANC


Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa Jumamosi January 12 mwaka huu, amezindua kampeni ya chama cha ANC ya uchaguzi wa bunge mwezi Mei, akikiri chama kufanya makosa hapo nyuma na kuahidi kurejesha taasisi za demokrasia.

Ramaphosa  aliwasilisha  manifesto yenye  kurasa  68 mbele  ya mamia kwa maelfu ya waungaji  mkono chama hicho katika mji wa  mashariki mwa Durban, akizindua  miezi  minne  ya  kampeni.

Chama  cha  African National Congress  ANC, ambacho kimetawala nchi hiyo tangu kumalizika  kwa  utawala wa kibaguzi miaka 25 iliyopita, kinatarajiwa kushinda uchaguzi huo licha ya kupungua kwa uungwaji mkono, migawanyiko ya ndani pamoja na uchumi usio na  kasi ya ukuaji.

Chama  cha  marehemu  Nelson  Mandela  kiliathirika kwa kupungua uungwaji wake mkono chini  ya urais uliokumbwa na kashfa telewa rais Jacob zuma, ambaye  aliondolewa Februari mwaka jana baada ya  uwapo  madarakani kwa miaka tisa.

"tunapaswa  kukiri kwamba  makosa  yalifanyika," ramaphosa alisema, na  kuongeza: "Baada  ya  kipindi cha  shaka  na  hali  ya sintofahamu, tumewasili  katika  wakati wa  matumaini  na  ujenzi mpya.

"Uchaguzi  wa  mwaka  2019 unatoa fursa  ya  kurejesha  taasisi zetu  za  kidemokrasia  na  kuirejesha  nchi  yetu  katika  njia  ya mabadiliko, ukuaji  wa  uchumi  na  maendeleo."

Katika  uchunguzi  wa  maoni  ya  wapiga  kura  uliofanyika  hivi karibuni  na  kundi  la  IPSOS umetabiri  kwamba  ANC inaweza kupata  kiasi  ya  asilimia  61 katika  uchaguzi  wa  bunge  la  taifa na  majimbo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.