Header Ads

Ruby-Mwanzoni kabla sijapata mimba nilijua nikija kupata, basi sitaweza kufanya chochote
MWANADADA anayetamba na Ngoma ya Alele, Hellen George ‘Ruby’ amesema kwamba mimba aliyonayo haimzuii kufanya kazi kama alivyokuwa akifikiri awali.  Ruby aliiambia Mikito Nusunusu kuwa, kabla hajapata mimba alihisi labda akiipata atashindwa kufanya shughuli zake nyingine, lakini hali imekuwa tofauti kwani anapiga kazi kama kawaida.


“Mwanzoni kabla sijapata mimba nilijua nikija kupata, basi sitaweza kufanya chochote, nilidhani labda nitakuwa nachoka sana, lakini namshukuru Mungu hali imekuwa tofauti kwani baada ya kuipata sasa hivi napiga kazi kama kawaida na nitaendelea hadi nitakapojifungua,” alisema Ruby.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.