Header Ads

Serikali imejikita katika kuzuia na kuthibiti ugonjwa wa kifua kikuu -Waziri Ummy
DAR ES SALAAM:Serikali imetoa Takribani million 902 na LAKI TISA kwa ajili ya kununua magari 10 na pikipiki 35 ili kuongeza nguvu kwa waratibu na wasimamizi wa huduma ya afya kuweza kuwafikia watoa huduma katika mikoa yao kudhibiti maogonjwa ya kifua kikuu na ukoma.

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu ameeleza hayo leo jijini Dar es salaam ambapo amesema serikali imejikita katika kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu na ukoma ili kuweza kuwagundua wagonjwa na kuwapatia huduma ya matibabu.
Waziri Ummy amesema lengo lao ni kuwaibua wagonjwa wa kifua kikuu na kuwapatia matibabu hivyo utoaji wa vyombo hivyo vya usafiri kwa waganga na watendakazi wa afya vitawezesha kuongeza nguvu kwa watendaji wa afya.


Richard Rontoga ni mwakilishi kutoka shirika lisilo la kiserikali la Ujeruman amesema Shirika hilo lipo tayari kuendelea kusaidia ununuzi wa magari na pikipiki kwa gharama nafuu kwa ajili ya kazi.


Vyombo hivyo vya usafiri vimetolewa katika mikoa 10 na Halmashauri 35 ikiwemo Mikoa na Pwani, Songwe, Kilimanjaro, Lindi, Kagera, Tabora, Mtwara, Ruvuma, Rukwa na Ilala.

Pia serikali imetoa wito kwa wananchi kwenda vituo vya afya ili kupima na kupata matibabu kwani kifua kikuu kinatibika na kupona kabisa.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.