Header Ads

Tahadhari: Mapenzi Kwa Njia ya Mdomo Huongeza Hatari ya Kupata Kansa ya koo!

Kuna wale wanaoapa kwamba bila kuzama chumvini hawapati utamu wowote wa mapenzi. Hii ina wahusu. Nasema tena hii inawahusu!

Madaktari wameendelea kutoa tahadhari kwamba kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo wenyewe wanaita oral sex, inaongeza sana hatari ya kupata kansa ya koo. Hii inasababishwa na kupata maambukizi ya aina fulani ya virusi wanaitwa kwa kitaalam Human Papilloma Virus type 16 (HPV-16). Kwa mfano nchini Marekani kuna visa vipya 9000 vya wagonjwa wenye kansa ya koo ambao husababisha na virusi hawa kila mwaka!

Virusi hawa husababisha pia kansa ya shingo ya kizazi. Wanasayansi wameonya kwamba ikiendelea spidi hii baadae wagonjwa wenye kansa ya koo watazidi wale wenye kansa ya shingo ya kizazi.

Hatari kubwa iko kwa wale ambao wana wapenzi wengi, kule kuonja huku na huku , huwezi jua virusi utavipata kutoka kwa nani. Hata hivyo hatari iko chini kidogo kwa wanawake kulinganisha na wanaume.

Pia matumizi ya sigara yanaongeza uwezekano wa kupata kansa.

Kazi kwenu sasa, kusuka ama kunyowa.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.