Header Ads

Trump asema kutakuwa na mabadiliko katika viza

Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kutakuwa na mabadiliko katika viza za muda   kwa wafanyakazi (H1-B ). Viza hizo kawaida huombwa na mashirika ya Marekani yanapotaka kuajiri wafanyakazi wasomi na wenye vipaji kutoka mataifa mengine.

Rais Trump ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kwamba anawahakikishia wamiliki wa viza H1-B kwamba mabadiliko yatafanyika kufanya kuendelea kubaki Marekani na hata kupata uraia wa nchi hio iwe rahisi zaidi. Na kwamba anawashauri watu wenye vipaji na ujuzi mkubwa kuichagua Marekani kutekeleza fani zao.

Viza za H1-B inatoa nafasi kwa wahitimu wa elimu ya juu na mabingwa katika fani mbalimbali kufanya kazi nchini Marekani kwa muda.

Kila mwaka hospitali na mashirika ya utafiti hutoa viza hizo za H1-B karibu elfu 85.

Rais Trump wakati wa kampeni za urais aliahidi kuzifuta viza hizo za H1-B, kwani aliziita " Mpango wa kazi usio na thamani"

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.