Header Ads

Ubonge Wamtesa Aika Mareale wa Navy KenzoSTAA wa kike wa Bongo Fleva kutoka Crew ya Navy Kenzo, Aika Mareale amefunguka kuteswa na ubonge ambao kila kukicha unazidi baada tu ya kupata mtoto.  Akipiga stori Mikito Nusunusu, Aika alisema amekuwa akiteseka na ubonge alionao kwa sasa kwani haupendi na watu mbalimbali wamekuwa wakimshangaa na kumtaka aanze kufanya mazoezi kwani anapoteza mvuto.


“Siupendi ubonge nilionao kwa sasa, mashabiki wangu kibao wamenitaka nianze kufanya mazoezi kwa sababu kunenepeana huku napoteza mvuto. Nimepokea maoni yao na nitaya fanyia kazi maana nimejikuta nanenepa kutokana na uzazi,” alisema Aika.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.