Header Ads

Ulimwengu afunguka haya baada ya kupata kichapo kutoka kwa Simba


Straika Mtanzania anayecheza soka katika klabu ya JS Saoura, Thomas Ulimwengu amesema Simba wametumia faida ya Uwanja wao wa nyumbani kupata matokeo.

Ulimwengu ambaye amejiunga na timu hiyo hivi karibuni, ameeleza walizidiwa katika mchezo huo na faida ya Uwanja wa nyumbani imewapa Simba matokeo.

Saoura walipata kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Simba, Mpira ulionekana zaidi kuwa wa upande mmoja baada ya waarabu kuzidiwa kwa kila kitu.

Licha ya matokeo hayo, Ulimwengu amefunguka kuwa nao watajipanga vema katika mechi inayofuata ili kumalizana na Simba vizuri

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.