Header Ads

Uongozi wa Yanga wafunguka kuhusu Kamusoko


Uongozi wa klabu ya Yanga umeutolea ufafanuzi ujumbe wa kiungo wake Mzimbambwe, Thaban Kamusoko baada ya kuleta sintofahamu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kamusoko aliandika ujumbe ukieleza kuwashukuru wapenzi na mashabiki wa Yanga kwa upendo waliomuoneshea tangu ajiunge na timu hiyo, ambapo mashabiki wengi waliokomenti walielewa kuwa ameshaagana na mabosi wake na ikachukuliwa kuwa anaondoka Yanga.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari, Dismas Ten, ameibuka na kuutolea ufafanuzi kuwa Kamusoko aliandika na hakuwa na maana ya kuondoka.

"Si kweli, alichokiandika hakina maana ambayo wengi wametafsiri, bado ana mkataba na Yanga na ataendelea kuwepo" alisema Ten.

Ten ameeleza kuwa ifikie wakati mashabiki wasiwe wanakariri mambo pale mtu anapoandika ujumbe wa aina kama ile, kwani si kweli kuwa anaondoka

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.