Header Ads

UWAWATA (T) yatangaza Rasmi tarehe ya kufanya uchaguzi
DODOMA:Kamati teule ya kusimamia uchaguzi wa umoja wa waganga na wakunga wa tiba asili Tanzania (UWAWATA "T" ) imetangaza rasmi tarehe ya kufanya uchaguzi huo huku ikitoa muda wa siku 7 kwa wanachama wanaohitaji kugombea nafasi za uongozi kujitokeza kujaza fomu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dodoma mwenyekiti wa kamati hiyo bw Boniventure Mwalongo amesema uchaguzi huo umepagwa kufanyika april 2 mwaka huu ili kupata viongozi watakaouongoza umoja huo.

Amesema kuwa uchaguzi huo umelenga kutoa nafasi ya kupata viongozi wapya kutokana na sintofahamu zilizojitokeza kwa viongozi waliokuwepo hali iliyopelekea wanachama kutoridhishwa na mwendendo wa viongozi hao.


Amezitaja nafasi zilizo wazi ndani ya umoja huo kuwa ni kazi maalumu, oparesheni,ukaguzi, pamoja na nafasi zote za kitaifa na kwamba viongozi waliokuwa wakishikilia nafasi hizo tayari wamesimama kuanzia octoba 17 2018 huku akiwataka wanachama kudumisha amani na kuacha kuwatisha wenzake kwa lengo la kutaka kukwamisha ushiriki mpana katika uchaguzi huo.


Aidha amesema kuwa wapo watu waliokuwa wakiwatisha na kuwabaikizia mambo kadhaa waganga wasio na uelewa juu ya kanuni na taratibu za kiuendeshaji hivyo amesisitiza kuwepo kwa ulinzi mkali kutoka serikalini.


Mmoja wa waganga wa tiba asili bi Mwasafari Juma na aliyekuwa katibu wa umoja huo bw Lucas Joseph Mlipu wamesema kuwa uchaguzi huo utaleta tija iwapo watapatikana viongozi bora watakaosimamia kwa weledi majukumu yao.Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.