Header Ads

wapoteza maisha kutokana na hali ya hewa mbaya Ujerumani

Kutokana na hali mbaya ya hali ya hewa nchini Ujerumani, watu 3 wamepoteza maisha yao katika siku mbili zilizopita.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari,katika  jimbo la Bavaria kusini mwa nchi hiyo watu watatu wamepoteza maisha siku ya Alhamisi.

Kwa sababu ya theluji nzito, mwanamke mwenye umri wa miaka 54 ameripotiwa kupoteza maisha baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo wakati akisubiria usafiri kwa muda mrefu.

Polisi wamesema mvulana mwenye umri wa miaka tisa alikufa katika kijiji cha Aying karibu na Munich  baada ya kuanguka na kuviringita chini ya mti kutokana na theluji kali.

Majeshi ya Ujerumani yametangaza kuwa askari 350 wanasaidia wananchi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.