Header Ads

Zahera asema kuwa afurahishwa na sapoti ya mashabiki


Mwinyi Zahera ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga amefunguka kuwa anafurahishwa na sapoti ya mashabiki anayopata akiwa ndani ya Yanga hali inayomfanya afanye kazi kwa juhudi.

Zahera amesema mashabiki wa Tanzania ni tofauti na wa nchi ya Congo kwani kule kila ukanda una timu yake tofauti na ilivyo Tanzania.

"Mashabiki wanapenda mpira na wanapenda timu zao, wanazipa sapoti kwa hali na mali hali ambayo inanifanya niwe na furaha kuwa ndani ya Yanga na ardhi ya Tanzania," alisema Zahera.

Zahera amekuwa kipenzi cha mashabiki pamoja na wachezaji kutokana na namna anavyoibuka kifua mbele kwa kupindua matokeo kila anapozidiwa mbinu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.