Header Ads

Abiria wote wapoteza maisha baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka

Watu 5 wameripotiwa kufariki katika ajali ya ndege ndogo kaskazini magharibi mwa Nairobi nchini Kenya.

Hakuna yeyote aliyeokolewa katika ajali hiyo iliyotokea  eneo la msitu wa Makutano uliopo Londiani. Ndege hiyo  mali ya hifadhi ya taifa ya Maasai Mara ilikuwa ikitoka Ol Kiombo mji wa Turkana kuelekea Lodwar.

Taarifa ya polisi nchini Kenya inasema wanaume 3 na wanawake 2, watu 5 jumla waliokuwa katika ndege aina ya Cessna 206-5Y BSE wamepoteza maisha baada ya ndege hiyo kudodondoka. 4 kati ya 5 waliokuwamo katika ndege hiyo ni raia wa kigeni.

Polisi a vikosi vya uokoaji vipo eneo la tukio vikifanya uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.