Header Ads

Baraka Avamiwa Studio na Mwanadada Aliyesema Amemtapeli

Baraka Avamiwa Studio na Mwanadada Aliyesema Amemtapeli
Siku chache zilizopita moja ya wadada wa mjini walifumuka na kusema kuwa wametapeliwa na msanii Baraka the prince shilingi milioni tano ambazo alimpa kama zawadi kutokana na kumpenda lakini pa kutaka kumsaidia katika muziki.

Wawili hao walitegemewa kuingia katika mapenzi endapo wangekubaliana ilhali tayari Baraka alikuwa amekwisha chukua kiasi cha pesa walizokubaliana lakini cha ajabu hakufanya chochote kwa dada huyo zaidi ya kutumia pesa hiyo kununua gari.


Siku ya jana , baraka alikuwa studia ya Clouds media akitambulisha wimbo wake mpya ndipo ghafa mwanadada huyo alipotokea studio hapo bila taarifa ya Baraka wala waaandishi wa habari waliokuwepo eneo hilo na kuanza kudai pesa yake.

Huku akiongea kwa jazba , dada huyo alisema kuwa Baraka ni tapeli na muongo na anamdai pesa yake zaidi ya milioni 5 ambayo aliitaka muda huo la sivyo aache gari.

Mwanadad huyo aliejulikana kama Sex Dina alitaka kujua muafaka wa pesa yake kwa sababu tangu alipomtoa Baraka polisi  na kukubaliana kurudishiana pesa hiyo lakini Baraka hukuwahi kuonana na dada huyo wala kutaka kuwasiliana nae tena.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.