Header Ads

Dkt Kigwangalla -hatutaruhusu wanyama hai kusafirishwa kwenda nje ya nchi


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali haitaruhusu tena
usafirishaji wa wanyama pori hai kutoka Tanzania kwenda nchi nyingine

Waziri Kigwangalla amesema wanaenda kubadilisha sheria ili kupiga marufuku kabisa biashara hiyo.

"Niseme wazi kuanzia sasa hatutaruhusu wanyama hai kusafirishwa kwenda nje ya nchi na wale
waliokuwa wanafanya biashara hiyo watafute njia njingine," amesema.

Ametoa majibu hayo baada ya kuulizwa swali la nyongeza na Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu aliyetaka kujua kama Mei 2019 watanzania hasa kina mama wa kijiji cha Fanisi wilayani Muhenza wataweza kusafirisha vipepo nje ya nchi baada ya zuio la miaka mitatu liloweka kuonekana kumalizika tarehe hiyo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.