Header Ads

"Edu Boy nimemtoa mkoani" - Young Killer

"Edu Boy nimemtoa mkoani" - Young Killer
Msanii wa hip hop Bongo, Young Killer, amesema ameshangazwa na kauli ya Edu Boy kusema kwamba Baghdad amemfahamu yeye kupitia Edu boy wakati Young Killer ndio alimtoa Edu boy mkoani na kumleta Dar kufanya muziki.


Akizungumza na eNEWZ amesema kuwa wanahip hop nyuma yake wapo yeye sio wa mwisho hadi kufikia Baghdad kusema hivyo inawezekana kuna vitu ambavyo ameviona ndio maana vikampelekea yeye kusema hivyo hata hivyo amemshukuru kwa kumuona yeye kuwa anafanya vizuri hadi kufikia kumtaja.

"Sioni kama hakuna kwa mtazamo wangu inawezekana yeye hadi kusema hivyo kuna vigezo ameviona, ila pia Bahgadad  ni mdau mkubwa wa muziki wa hip hop pia ni mtangazaji na msanii  hivyo hadi kusema hivyo ni kwamba kuna vitu tayari ameviona kwangu ndio maana akasema lakini mimi naona wapo wengine waliokuja nyuma yangu na wako poa tu ", alisema Young Killer.

Akizungumzia maendeleo ya muziki wa hip hop, Young Killer amesema kuwa bado katika tasnia wanahitajika wana hip hop halisi ili waweze kuukomboa muziki huo.

Pia amemalizia kwa kusema kuwa yeye ndiye aliyemshawishi  Edu Boy kufanya muziki na alimtoa shule na kuamleta Dar kufanya muziki hivyo kwa sasa anayoyazungumza ni sawa kwa kuwa kila mtu ana uhuru wa kuzungumza.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.