Header Ads

Eto’o agoma kustaafu soka

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o amenukuliwa na mtandao wa BBC akisema, ataendelea kucheza na hana wazo la kustaafu kwa saaa.

Eto’o kwa sasa anacheza nchini Qatar soka la kulipwa na amesema atasfaafu pale atakapohisi mwili wake haumruhusu tena kuendelea kucheza.

“Ana hoja ndani yake na unaweza kuona ni kitu cha tofauti, kuna wachezaji kama Michael Essien, Yaya Toure ambao waliibuka baada ya Eto’o lakini leo tayari kama wamemaliza kila kitu lakini Eto’o bado anatwanga japo sio katika kiwango ambacho alikuwanacho Barcelona na Inter Milan”-Geoff Lea

“Anacheza au anafanya biashara? Eto’o anafanya appearances Qatar hashindani tena wengine wanaamua kutulia na kufanya mambo mengine lakini yeye ana sababu nyingine ya ziada inayomfanya endelee kubaki kwenye mpira na mimi namuelewa”-Shaffih Dauda.

“Kuna wachezaji wengine wanang’ang’ania kubaki kwenye mpira wa ushindani mfano Cristiano Ronaldo unaweza kujiuliza kwa nini bado anapambania UEFA Champions League wakati tayari ana medali kibao wakati angeweza kwenda China kupiga mihela wakati kina Eto’o mapema walikimbia kwenda Urusi na kuwa mchwzaji anaelipwa kiasi kikubwa cha pesa kuliko mchezaji yeyote katika dunia hii.”

“Mtu kama Eto’o kwake mkwanja ndio kipaombele na mimi nakubaliana nae kwa sababu familia za Afrika kuna mahitaji makubwa ya pesa na wakati yupo timu ya taifa alikuwa anatoa bonus kwa wachezaji wenzake endapo timu inapata ushindi.”

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.