Hizi ndizo Bidhaa za chakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa Bei wa mwezi Januari ,2019
![]() |
DODOMA.Imeelezwa kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa Mwaka ulioishia mwezi januari , 2019 umepungua
hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 3.3
kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba mwaka 2018.
Hayo
yamesemwa na Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa sensa ya watu na Takwimu za jamii Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Hapa.
Aidha,
kwesigabo ameongeza kuwa kupungua kwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka
ulioishia mwezi Januari , 2019
kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za bidhaa za vyakula kwa kipindi
kilichoishia mwezi januari ,2019 zikilinganishwa na bei za mwaka ulioshia mwezi
januari, 2018 huku mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi januari ,2019 umeendelea kupungua hadi
asilimia 0.7 kutoka asilimia 1.0
ilivyokuwa mwezi disemba , 2018.
Mbali
na hilo amesema Baadhi ya Bidhaa za chakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko
wa Bei wa mwezi Januari ,2019 ni pamoja na mchele kwa asilimia 3.9, mahindi
13.9, unga wa mahindi kwa asilimia 8.9 , mtama kwa asilimia 5.1, unga wa muhogo
kwa asilimia 6.8, maharage kwa asilimia 4.2, choroko kwa asilimia 10.5, mihogo
mibichi kwa asilimia 5.6 viazi vitamu kwa asilimia 3.3, magimbi kwa asilimia
18.6 na ndizi za kupika kwa asilimia 13.3.
Katika
hatua nyingine amesema hali ya mfumuko wa Bei kwa nchi za afrika mashariki
ambapo Nchini Kenya mfumuko wa bei kwa
mwaka uliishia mwezi januari ,2019 umepungua hasi asilimia 4.70 kutoka
asilimia 5.71 kwa mwaka ulioishia mwezi disemba, 2018 na kwa
upande wa Uganda mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi januari ,2019 umeongezeka hadi asilimia
2.7 kutoka asilimia 2.2 kwa mwaka ulioishia
mwezi Disemba mwaka ,2018
Hatahivyo,
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa sheria ya
takwimu ya mwaka 2015, kwa mujibu wa sheria hiyo NBS imepewa
mamlaka ya kutoa na kusimamia na kuratibu upatikanaji wa Takwimu Rasmi Nchini ikiwa ni pamoja na
takwimu za mfumuko wa bei kwaajili ya
matumizi ya serikali na wadau wa takwimu.
Na jackline victor kuwanda
No comments:
Post a Comment