Header Ads

Kaburi jingine la halaiki lagunduliwa

Katika jimbo la Colima magharibi mwa Mexico kaburi ambalo ndani yake walizikwa watu wengi lagunduliwa.

Taarifa zinasema kwamba miili 50 ilipatikana kwenye kaburi la siri katika kipande kimoja cha ardhi katika kata ya Santa Rosa.

Zoezi la kuitambua miili hiyo limeanza. Wiki iliyopita kaburi jingine la siri lililokuwa na miili 19 liligunduliwa eneo hilohilo.

Kwa mujibu wa takwimu za Mexiko, Mwaka 2017 jimbo la Colima ndio linaloongoza kwa kesi za mauaji kwa kuripoti kesi za mauaji 113 katika kila watu laki moja

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.