Header Ads

Kimenuka...Unaambiwa Kila Anayeingia ‘Guest’ Njombe Lazima awe na Kitambulisho

Watu wote wanaoingia kwenye nyumba za kulala wageni Njombe ni lazima waonyeshe kitambulisho kinachotambulika na Serikali.

Mkuu wa wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amesema kila aneyeingia Njombe awe na kitambulisho huku akisema kuwa anaamini hakuna mtu atakaesema hana kitambulisho cha mpiga kura au cha Taifa.

“Katika kipindi hiki tuhakikishe tunajisimamia maeneo yetu tunayoishi. Mgeni yeyote iwe ni kijijini au mjini tutoe taarifa kwa viongozi wetu na kwenye nyumba za kulala wageni tumeshatoa maelekezo.”

“Kila anayeingia nyumba ya kulala Njombe hii awe na kitambulisho ninaamini hakuna mtu atasema hana kitambulisho cha mpiga kura au cha taifa kama huna basi wewe si raia wa Tanzania,” amesema Msafiri.

Mkuu wa Wilaya hiyo ametoa kauli hiyo leo Jumamosi wakati akizungumza na maofisa ustawi wa jamii ngazi ya wilaya na kata katika semina ya Kamati ya Ulinzi wa Mwanamke na Watoto iliyokuwa ikitolewa na maofisa kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto.

Semina hiyo pia ilitoa mafunzo ya na namna ya kukabiliana na matukio ya utekaji na mauaji ya watoto yanayoendelea wilayani Njombe

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.