Header Ads

Kocha Julio Ajitetea Kwenye Kashfa ya Rushwa Dodoma FC

Kocha wa Dodoma FC Jamhuri Kihwelo Julio amekana timu yake kuhusika na suala la kutoa rushwa ili kushinda mchezo dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora, huku akisema hajawasiliana na Waziri Mkuu kama ilivyodaiwa na viongozi wa Rhino.


Julio ameiambia www.eatv.tv kuwa sio rahisi kwake kuonana na Waziri mkuu hivyo wao wanategemea matokeo ya uwanjani na sio mambo ya kutoa rushwa.

''Huwezi kukutana na Waziri Mkuu kirahisi hivyo, wao tumewaambia ulinzi uongezwe uwanjani maana tumeona timu nyingi hapa zimepigwa na mashabiki kwahiyo wameleta chuki'', amesema.

Aidha Julio amesema taarifa hizo zinalengo za kuwachafua kwani wapo hayo mambo huwa hawafanyi na ndio maana wanapoteza mpaka michezo ya nyumbani hivyo hawawezi kununua ya ugenini.

Mbali na hilo Julio amesema hajakutana na Waziri mkuu Kassim Majaliwa kwaajili ya kuomba ulinzi wala mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ambaye naye ilidaiwa alikwenda kuonana naye.

Kwa upande wa TFF wao wamesema wanafuatilia suala hilo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.