Header Ads

Kocha wa Simba SC aeleza mbinu aliyotumiwa kuwanyamazisha Al Ahly

Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems ameeleza mbinu aliyotumia kuwanyamazisha wapinzani wao Al Ahly kwenye mchezo wa Klabu Bingwa Afrika.

Patrick Aussems amesema kuwa walifahamu fika wapinzani wao walikuwa na hofu, hivyo wakaamua kutumia muda mwingi kuwashambulia.

“Tulianza kwa kuwashanbulia tangu mwanzo sababu tulijua mabeki wao wana hofu kwahiyo tulijaribu kuwaweka katika matatizo, na tunashukuru tulifanikiwa kufunga goli kipindi cha pili,”
amesema Kocha Patrick Aussems.

Hapo jana wekundu wa Msimbazi, Simba SC katika dimba la Uwanja wa Taifa Dar es Salaam waliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Al Ahly kutoka Misri na kuwafanya kufikisha pointi 6 katika kundi lao.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.