Header Ads

'Maharlika' ndio jina linalofikiriwa kupewa Taifa la Ufilipino

Imefahamishwa kwamba Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte anafikiria mpango wa kubadilisha jina la nchi yake kuwa "Maharlika".

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya Ufilipino Duterte alifahamisha kwamba wanataka wabadilishe jina la nchi lililotolewa na kipindi cha utawala wa kikoloni na mfalme wa Hispania ,Felipe II, na kuipa nchi jina jipya la "Maharlika"

Naye msemaji wa ofisi ya rais nchini humo Salvador Panelo alitoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari kwamba Rais Rodrigo Duterte alizungumzia uwezekano wa kubadilisha jina la nchi hiyo.

Maharlika ni neno la lugha ya Kimalay hivyo jina hilo litaakisi asili ya Malay ya taifa hilo.

Wazo la kubadilisha jina la nchi hio kuwa Maharlika lilitolewa kwa mara ya kwanza na rais wa zamani wa nchi hiyo Ferdinand Marcos.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.