Header Ads

Makambako Wakumbwa na Uhaba wa Kondom..... Madiwani Wampa Siku Saba Mkurugenzi Kushughulikia

Makambako Wqkumbwa na Uhaba was Kondom..... Madiwani Wampa Siku Saba Mkurugenzi Kushughulikia
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe limetaarifu kuadimika kwa  Kondomu kote madukani halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe  hivyo kuwaagiza wataalamu wake kutafuta mwarobaini kwani ni kikwazo katika jitihada za kukabiliana na maradhi ya Ukimwi.

Wajumbe wa Baraza hilo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hanana Mfikwa walisema licha ya kuadimika hata zile zinazopatikana zimekuwa zikiuzwa hadi Tsh 800 moja kiwango ambacho wanakitaja kutokuwa rafiki kwao.

Madiwani  wa kata mbalimbali  katika Halmashauri ya Mji wa makambako wamekutana katika kikao cha baraza la madiwani kujadili masuala ya maendeleo,lakini Baada ya kamati ya kudhibiti UKIMWI  kuwasilisha taarifa zake madiwani walisimama na kuhoji juu ya upungufu wa kinga katika halmashauri hiyo

Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Makambako Ernest Kiungu alisema kwa muda sasa wahisani ndio wamekuwa wakisambaza mipira hiyo ya kiume lakini kwa sasa  Bohari ya dawa ya Mjini Iringa haijatoa kinga hizo.

Aidha Baraza la madiwani limempa muda wa  siku saba mkurugenzi wa halmashauri hiyo Paul Malala  kuhakikisha kinga zinapatikana katika maeneo yote yanayopaswa kuwapo ili kunusuru afya za wananchi.

Inaelezwa Kinga zimeadimika katika nyumba za kulala wageni ,zahanati , vituo vya afya na katika maeneo mengine hali ambayo inakuwa changamoto katika kukabiliana na maambukizi ya ukimwi katika mkoa wa Njombe ambao ni kinara nchini kwa maambukizi kwa asilimia 11.8.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.