Header Ads

Mbona tunaanza kusutana? 2020 Mavunde atapita bila kupingwa - Mbunge Ditopile


Mbunge wa viti maalum (CCM) Mariam Ditopile, amewataka wananchi wa Dodoma kumpongeza Mbunge wao Antony Mavunde, kwa juhudi kubwa alizozifanya za kuhakikisha serikali inatoa punguzo kubwa kwenye zao la Zabibu.

Ditopile amesema kuwa Wabunge wakiona mambo yanaenda vizuri waongezee nyama na sio kusutana sutana ili mambo yaweze kwenda sawa.

"Mbunge wangu wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde ambaye anajinasibu kwa watu kuwa yeye ni mtu wa watu, aliomba Punguzo la zabibu mbele ya Rais na Waziri Mkuu, hakusita kuna siku nimemabana nae mpaka ofisi za TRA akiomba punguzo hili hawezi kujisemea humu ndani," alisema Ditopile Bungeni jijini Dodoma.

"Fadhila kwa watu wa Dodoma mumrudishe Mbunge wenu aliwasemea na kweli amehakikisha yeye ni mtumishi wenu, Mh. Spika atapita bila kupingwa hilo linajulikana."

"Mnasema mbona tunaanza kusutana, mmeongea mmesikika mambo yamerekebishika mnaanza ooh Mpango amesikia asingesikia mngerekebisha nini? kama mambo yanaenda vizuri tuendelee kusifia tuongezee nyama sio tunaanza tena kusutana sutana," aliongeza

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.