Header Ads

mwanamke auwawa na nguruwe aliokuwa akiwafuga


Mwanamke mmoja nchini Urusi ameauawa na nguruwe aliokuwa anawafuga baada ya kuanguka kwenye banda la wanyama hao.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Urusi, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 56 alikuwa akiwalisha nguruwe ndipo ghafla akaanguka na nguruwe hao wakamtafuna.

Inasadikiwa kuwa chanzo cha kuanguka kwake ilikuwa ni kuzirai ama kupatwa na kifafa, Tukio hilo limeripotiwa kwenye wilaya Malopurginsky jimboni Udmurtia, lililopo katikati ya Urusi.

Vyombo vya habari vya urusi vinaarifu kuwa mume wa marehemu alikuwa amelala wakati mkewe alipokuwa akiwahudumia nguruwe hao. Bwana huyo inasemekana alikuwa mgonjwa.

Baada ya kuamka alianza kumtafuta mkewe na kukuta mwili wake ndani ya banda la nguruwe, Inataarifiwa kuwa alifariki baada ya kupoteza damu nyingi. Tayari upelelezi jwa polisi juu ya tukio hilo umeshafunguliwa

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.