Header Ads

Ombi la Bilionea Mo Dewji kwa mashabiki wa Simba SC


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simba SC,Mohammed Dewji amesema timu yao ina nafasi ya kufanya vizuri licha ya matokeo mabaya iliyopata hivi karibuni.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Dar es Salaam amewataka washabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa timu hiyo wiki ijayo dhidi ya Al Ahly

"Niwaombe Wanasimba wasivunjike moyo, wote tumeumia lakini huo ndio mchezo. Lakini mimi naona bado tuna nafasi, tumeshawahi kuzifunga timu nyingi za kiarabu hapa Dar es Salaam," amesema Mo.

"Ninaamini kama tukijitokeza kwa wiki kuishangilia timu yetu siku ya Jumanne tutafanya vizuri na mimi nitakuwepo uwanjani," amesema.

Hadi sasa Simba SC ina pointi tatu katika michezo mitatu iliyocheza, ikiwa imefunga magoli matatu pekee, huku ikiruhusu jumla ya magoli 10 katika michezo miwili ya mwisho kucheza dhidi ya AS Vita kutoka DR Congo na Al Ahly ya Misri.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.