Header Ads

Ray c afunguka haya kuhusu wimbo wake mpya

Mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema wimbo wake mpya wa ‘Umezima’ ni zawadi maalumu kwa mashabiki wake katika msimu wa Valentine.

Msanii huyo amesema ameamua kuwapa burudani ya Valentine mashabiki ambao kwa muda mrefu wamekuwa na shauku ya kusikia zaidi kazi zake.

“Huu ni mwendelezo wa ujio wangu kwenye tasnia hii tena, natambua mashabiki watakuwa na shauku ya kunisikia zaidi, lakini niwajulishe tu nitaendelea kutoa kazi juu ya kazi ili kuwapa burudani,” alisema Ray C.

Mwanadada huyo ambaye ameonekana kurudi vema kwenye tasnia ya muziki, amesema anafarijika kusikia na kuona mashabiki wakipokea kazi zake.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.