Serikali yajipanga kwa hili
Serikali
imesema haitakua tayari kuona Amani na Utulivu wa Nchi inachezewa huku
ikisisitiza uwepo wa Umoja kati ya wananchi bila kujali tofauti ya
imani, kabila au itikadi yoyote.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni wakati akifungua Semina ya siku mbili iliyofanyika jijini Dar es
Salaam ikiwahusisha Viongozi wa Taasisi za Kiislamu lengo ikiwa ni
kuwakumbusha kuhubiri amani katika sehemu zao
Amesema
muelekeo na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kukuza maendeleo
katika sehemu mbalimbali nchini lengo ikiwa kuinua maisha ya wananchi
nan chi kwa ujumla
“Serikali
hii imejidhatiti kuhakikisha maendeleo yanakuja kwa kasi na maendeleo
hayawezi kuja ikiwa amani na utulivu haupo, sisi kama serikali
tutahakikisha tunalinda amani iliyopo ili wananchi wapate kufanya
shughuli za kiuchumi bila wasiwasi wowote” alisema Masauni
Akizungumza
wakati wa ufunguzi huo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa
Salum aliihakikishia serikali kutokuwepo kwa mifarakano kati ya taasisi
mbalimbali kama ilivyokuwepo awali huku akisisitiza kuendelea kwa umoja
huo ili jamii ipate kuendelea
“Sisi
kama Bakwata tunaihakikishia serikali uwepo wa umoja na ushirikiano
baina ya baraza na taasisi zingine na tofauti zetu hazipelekei kukoseana
au kuvunjiana heshima kwahiyo tunaomba serikali iamini uwepo wa
maelewano mazuri tu kwa maendeleo ya nchi hii” alisema Sheikh Mussa
No comments:
Post a Comment