Header Ads

Serikali Yataka kodi ya Majengo kuwa Sh10,000 kwa majengo ya mijini na vijijini.

Serikali imewasilisha marekebisho ya viwango vya kodi vya majengo ya kawaida kuwa Sh10,000  kwa majengo ya mijini na vijijini.

Marekebisho hayo yamewasilishwa chini ya marekebisho ya Sheria Mbalimbali namba 2 wa mwaka 2019,  jana  Februari 9, 2019 na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  Profesa Adelardus Kilangi.

Profesa Kilangi amesema Serikali inapendekeza marekebisho ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya utozaji wa Kodi ya Majengo lengo likiwa ni kiwango mfuto (flat rate) vya kodi ya majengo na kuiwezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa mkusanyaji pekee wa kodi ya majengo.

“Viwango vinavyopendekezwa ni Sh20,000 kwa nyumba za ghorofa katika maeneo ya vijijini na Sh50,000 kwa kila sakafu kwa nyumba za ghorofa katika maeneo ya mjini,”amesema.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.