Header Ads

Shilole amwaga povu kwa wasanii kisa hiki

Shilole Awataka Wasanii Waache Unafiki Wa Kusapotiana Baada Ya Kifo
Shilole Awataka Wasanii Waache Unafiki Wa Kusapotiana Baada Ya Kifo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameibuka na kuwajia juu wasanii ambao wameonekana kusapoti na kulilia wasanii wenzao Baada ya kifo.

Siku ya jana Msanii wa muziki wa hip hop nchini Godzillah alifariki dunia Baada ya kuugua ghafla nyumbani kwake Salasala. Wasanii mbali mbali walijitokeza kutoa pole na hata kumposti katika kurasa zao ya Mitandao ya kijamii.


Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Shilole amewajia juu baadhi ya wasanii ambao amediriki kuwaita wanafki na kudai wamejitokeza Baada ya kifo chake na kuanza kumposti na kudai wameguswa wakati kwenye uhai wake hakuna hata mmoja aliyeposti kazi zake.

Mimi naona ni vizuri mtu akapewa heshima yake wakati yuko hai ili aone kama kuna watu wanampenda na kumjali sasa Leo hii amekufa ndio anapewa hio sapoti anajuaje sasa?

Wakati yupo hai anatoa nyimbo hamposti wengine Mpaka wanatumia ngoma zake kama cover lakini bado hawamposti wala kumpa heshima yake kama legendari Ndio maana  mimi kila siku nasema wasanii tuache unafiki wengi watu ni wanafiki sana”.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.