Header Ads

Simba SC wapewa dawa kuepuka vipigo Klabu Bingwa Afrika


Wakati kikosi cha Msimbazi, Simba SC kikiwa na kazi kubwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo hakijafanya vizuri kwenye michezo yake miwili ya mwisho, kikosi hicho kimeendelea kupewa maoni na wadau wa soko nchini.

Sasa ni Kocha wa Lipuli, Seleman Matola ambaye amesema kuwa kikosi hicho kinahitaji
maboresho makubwa hasa katika safu ya ulinzi.

"Benchi la ufundi linapaswa liangalie kwa ukaribu sehemu ya ulinzi namna ya kufanya
maboresho ili wasiruhusu mabao mengi kwani kufungwa sana kunamanisha kuna njia ya kupita hasa kwa upande wa mabeki, nafasi ya kufanya vizuri ipo kwani kundi lao bado lipo wazi,"
amesema kocha huyo.

Hadi sasa Simba SC ina pointi tatu katika michezo mitatu iliyocheza, ikiwa imefunga magoli matatu pekee, huku ikiruhusu jumla ya magoli 10 katika michezo miwili ya mwisho kucheza dhidi ya AS Vita kutoka DR Congo na Al Ahly ya Misri ambayo itarudiana nayo wiki ijayo uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.