Header Ads

Sitaki Kufananishwa na Sanchi”- Poshy Queen

“Sitaki Kufananishwa na Sanchi”- Poshy Queen
Mrembo anayekimbiza kwenye Mitandao ya kijamii kutokana na umbo lake matata Jackline Obeid maarufu kama Poshy Queen ameibuka kutaka asifananishwe na watu wengine.

Poshy amefunguka na kusema kuwa hataki kufananishwa na mrembo mwingine ambaye anatengeneza headlines kila siku kwa umbo lake matata anayejulikana Kama Sanchi.

Katika mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Sanchi amefunguka na kusema kwamba hataki kufananishwa na Sanchi kwani yeye binafsi haoni kama wamefanana.

Naomba niweke hiki kitu ili kiwe clear sidhani kama ni sawa kunifananisha mimi na watu kwanza hatufanani, hatuna undugu sio marafiki na hata mtu akituangalia hatufanani kwanza hata shepu zetu hazifanani halafu mimi ni mrefu kwake kwaiyo hatuendani”.

Sanchi na Poshy Queen wamekuwa wakifananishwa kutokana na wote wawili kuwa na maumbile makubwa Lakini pia wote wamekuwa wakiachia picha tata kwenye Mitandao ya kijamii.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.