Header Ads

Tetema ya Rayvanny yashindwa kuvunjwa rekodi ya Diamond

Tetema ya Rayvanny yashindwa kuvunjwa rekodi ya Diamond
Wimbo mpya wa msanii Rayvanny na Diamond Platnumz 'Tetema' unazidi kufanya vizuri mara
baada ya video ya wimbo huo kutoka.

Video ya wimbp huo imeweza kufikisha watazamaji (views) Milioni 1 kwenye mtandao wa YouTube
ndani ya saa 17 pekee.

Hata hivyo Rayvanny ameshindwa kuifikia rekodi ya Diamond kupitia wimbo wake 'Hallelujah'
aliowashirikisha Morgan Heritage ambao ulifikisha watazamaji Milioni 1 ndani ya saa 15 pekee.

Utakumbuka September 2016 video ya wimbo, Salome ambao Diamond alifanya na Rayvanny uliweza kufikisha watazamaji Milioni 1 ndani ya siku mbili pekee rekodi ambayo ilikuja kuvunjwa na wimbo wa Alikiba ambao ulifikisha idadi hiyo ya watazamaji kwa saa saa 37.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.