Header Ads

Ummy-anaume wasiotahiriwa wana uwezekano wa kuambukizwa saratani ya kizazi


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema tohara imekuwa wenyewe manufaa zaidi kwa kuwaepusha watu na magonjwa na kuitaka jamii kutoipuuza.

Hapo jana Bungeni mbunge wa Viti Maalum CCM Jacqueline Msongozi alieyeshauri Bunge kuanzisha utaratibu wa kuwafanyia tohara Wabunge wa kiume ambao bado hawajafanyiwa huduma hiyo.

Waziri Ummy amesema tohara ina umuhimu wake kwani utafiti unaonyesha kuwa inapunguza uwezakano wa kupata virusi vya Ukimwi kwa asilimia 60.

"Utafiti wa kitaalam umebaini pia wanaume wasiotahiriwa wana uwezekano wa kuambukizwa saratani ya kizazi," amesema.

Waziri Ummy pia amesema kuwa serikali imetoa kipaumbele kwa kutoa huduma ya tohari bure kwa wanaume ambao hawajafanyiwa katika mikoa 17 nchini. Baadhi ya mikoa hiyo ni kama Iringa, Njombe, Tabora, Mbeya, Rukwa, Katavi na Geita.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.