Header Ads

Viwanda 3,500 vyaanzishwa nchini ndani ya miaka mitatu


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya amesema jumla ya viwanda 3,504 vimeanzishwa nchini na serikali ili kujenga uchumi wa viwanda.

Amebanishha hayo Bungeni alipokuwa  akijibu swali la mbunge wa Chumbageni, Ussi Salum aliyetaka kujua viwanda vingapi vimeanzishwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano ianze utekelezaji wa mpango wa kuimarisha uchumi wa kati wa viwanda.
“Kati ya viwanda hivyo 3,504 vilivyoanzishwa, vinajumuisha viwanda vidogo sana 2,500, viwanda vidogo 943, viwanda vya kati 51 na viwanda vikubwa 10,” alisema.

Mhandisi Manyanya alisema wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina imekuwa ikifanya tathmini ya viwanda 156 vilivyobinafsishwa na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kwa viwanda  68  ambavyo havijaendelezwa.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.