Header Ads

Wanaharakati Zanzibar Watoa tamko hili
Wanaharakati kutoka Asasi za kiraia zipatazo 10 Zanzibar zimetoa tamko la kuviomba vyombo vya dola kuchukua hatua za haraka kwa maofisa wa jeshi la polisi wanaodaiwa kuhusika na kuvamia na kudhalilisha Maofisa wa Mamalaka ya kupambana na rushwa na kuhujumu uchumi Zanzibar (ZAEC).


Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mohamed wakati akitoa tamko la pamoja la asasi za kiraia zipato 10 juu ya tukio la uvamizi lilifanywa na jeshi la polisi dhidi ya mamalaka ya kuzuia rushwa na kuhujumu uchumi Zanzibar mnamo Februari 4 mwaka huu.

Bi.Jamila alisema vyombo vya dola vinatakiwa kuhakikisha wanasimamia sheria ipasavyo  kwa kuwachukulia hatua za kisheria kwa wale maofisa wa polisi wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo.

"Kesi hii inapaswa ishughulikiwe kisheria na si kwa njia ya mazungumzo kwani kitendo kilichofanywa ni cha kwa nchi na chombo cha dola kama vile jeshi la polisi," alisema Bi. Jamila.

Aidha alisema hutua hiyo ya kuwajibisha maofisa hao wa jeshi la polisi itapelekea haki kutendeka na itakuwa fundisho kwa maafisa wengine wanaotumia nguvu kulinda maslahi yao kwa kukiuka sheria.

Tukio hilo lilitokea mara baada ya Maafisa wa Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi kumuwekea mtego mmoja wa askari wa jeshi la polisi.

Ambapo alipobainika kuhusika na kumshika na Rushwa jambo ambalo limechochea hasira kwa jeshi hilo kutokana na mwenzao huyo kukamatwa na mtego na kwenda kutoa kichapo kwa maafisa.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.