Wasafirshaji wa mirungi waja na mbinu mpya
WAFANYABIASHARA
na Wasafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi wamekuja na mbinu
nyingine mpya ya kujigeuza wanafunzi na kisha kuficha Mirungi katika
mabegi madogo yanayotumiwa na wanafunzi kuhifadhi Daftari kwa lengo la
kukwepa mkono wa askari Polisi.
Mbinu
nyingine ambazo jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro imezigundua hivi
karibuni ni pamoja na kutumia magari ya Kifahari yakiwemo Toyota Land
Cruser ,Toyota Alphasad,Toyota Vanguard huku mbinu nyingine zikiwa ni
kufanyia mabadiliko gari aina ya Toyota Noah ili kurahisisha ubebaji wa
Mirungi kwa kificho.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issah
alisema wasafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi wameendelea
kubuni mbinu kila kukicha baada ya zile za awali kushtukiwa na Polisi
huku akitoa onyo kwa wamiliki wa Magari ya abiria kujiingiza katika
mtego wa kusafirisha dawa hizo.
“Hapa
kuna mizigo ambayo imekamatwa na askari wetu wakiwa barabarani ,hii ni
mbinu mpya ya usafirishaji ,haya mabegi unayoyaoona yote ni mabegi
yanayoonesha mbebaji amebeba Madaftari anaenda shuleni ,lakini haya sio
madaftari ni Mirungi ,ni mizigo iliyokamatwa kwenye mabasi tofauti
tofauti”alisema Kamanda Issah.
Alisema
katika tukio hilo watuhumiwa tisa wakiwemo wanawake wawili wamekamatwa
wakiwa na jumla ya kilogramu 64 baada ya sakari Polisi kupekuwa magari
matatu ya Abiria yaliyokuwa yakitokea yakiendelea na safari kutokea
Moshi yakielekea Arusha.
“Naona
mbinu zinaendelea kubadilika ndani ya wiki mbili ,mbinu tatu
tofauti,kwanza ya kujaza kwenye magari,pili ya kutoboa magari
kabisa,tatu kama mwanafunzi nyingine kama mtu anaenda hospitali
amejifunga maplasta sasa hizi mbinu zitafika mpaka lini na sisi
tunashukuru askari wangu wanafanya kazi vizuri”alisema Kamanda huyo wa
Polisi Kilimanjaro.
Kamanda
Issah amewataja wanaoshikiliwa hadi sasa kuwa ni pamoja na Ibrahim
Masuli, Godfrey Richard, Chrispin Baltazar, Fanuel Hamad,na Jackline
Mushi huku wengine wakiwa ni Lucy Petro ,Nuru Haruna,Silvesta Fabian
naMinyari Miandei.
Alisema
kwa sasa askari polisi wameamua kupekuwa magari yote yakiwemo ya abiria
huku akiwataka abiria kutoa ushirikiano kwa jeshi l a Polisi pindi
wanapoona mizigo yenye mashaka ili kuwaondolea adha ya kuchelewa kufika
safari zao kutokana na usumbufu watakao pata barabarani.
“Tunawasihi
abiria maana kuna abiria wengine wakiona askari wanapekua gari
wanakasirika,msikasirike hii ndio kazi ya kupekuwa ,vinginevyo muwe
mnatuambia ndani ya gari amepanda mtu wa ajabu na amebeba madawa ya
kulevya aina ya mirungi hapo ndio itakuwa ni nanafuu na tutafanya kazi
kwa muda mfupi li muendelee na safari “alisema Issah.
Kamanda
Issah aliwataka wamiliki wa mabasi ya abiria kutoa ushirikiano kwa
jeshi la polisi ili kuhakikisha biashara hiy inakoma kwa kukataa kubeba
abiria wenye mizigo ambayo wanatilia shaka na kwamba kwa kuendelea
kuwabeba itapelekea kuwaingiza katika matatizo na vyombo vyao.
“Sasa
hivi sio imekuwa ni wanafunzi ambao madaftari yao ni mirungi iliyobebwa
nyuma ,kwa hali kama hiyo tunawasihi wale wote wasafirishaji wa abiria
kutokea Moshi kwenda Arusha wawe makini utawachelewesha abiria
wako,upekuzi utaendelea na ninaelekeza askari waendelee usiku iwe
mchana”alisema Issah.
“Kuna
watu wakiona gari inapekuliwa wanatubeza ,sasa hivi tukikuona wewe
unatubeza askari watakukamat,a wanawabeza askari wanaofanya kazi yao
halafu tutakuhoji unatubeza kwa sababu gani,kwa hali kama hiyo tunaagiza
askari waendelee kukamata mirungi na wasiiache”aliongeza Kamanda Issah.
No comments:
Post a Comment