Header Ads

Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye Aumwa ghafla .


Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ameumwa ghafla akiwa Mkoani Tanga katika shughuliza chama.

Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene amesema kiongozi huyo ambaye pia mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho amekimbizwa Hospitali ya Bombo na kupatiwa matibabu na inaelezwa kuwa hali yake inaendelea vizuri.

Ameongeza kuwa kwa sasa kunafanyika mipango ya kumsafirisha kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

Januari 11, 2016 Rais John Magufuli alikwenda kumjulia hali Sumaye katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipokuwa akitibiwa kwa wakati huo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.