Header Ads

Waziri Ummy aunga mkono hoja ya wanaume kufanyiwa tohara, aja na tafitiWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka Watanzania kutoidharau hoja ya mbunge wa viti maalum (CCM), Jackline Ngonyani ya wanaume kufanya tohara ili kupambana na maambukizi ya virusi ya ugonjwa wa ukimwi.

“Utafiti wa kitaalam umebaini pia wanaume wasiotahiriwa wana uwezekano wa  kuambukiza saratani ya kizazi,” amesema Ummy.

Ummy amesema umuhimu wake unatokana na tafiti kuonyesha kuwa tohara kwa wanaume zinaweza kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa asilimia 60.

Waziri huyo alikuwa akijibu hoja za wabunge waliochangia taarifa ya kamati ya huduma na maendeleo ya jamii iliyowasilishwa bungeni leo.

Aidha amesema pia katika kuhakikisha kuwa suala la tohara linakuwa endelevu wameanzisha kampeni ya kufanya tohara kwa watoto wenye umri wa siku moja hadi siku 60.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.