Header Ads

Wenger afunguka kuwa muda wa furaha umekwisha kwa mtu huyu


Meneja mstaafu wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger amefunguka kuwa muda wa furaha umekwisha kwa meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer baada ya kupokea kichapo kutoka kwa PSG.

Wenger amesema kuwa Solskjaer alipata faida ya ushindi wa mwanzo kutokana na ratiba kuwa nyepesi kwake baada ya kuchukua nafasi ya Jose Mourinho.

"Takwimu muda mwingine zinaweza kudanganya. Kwa nini? Kwa sababu Rashford alipata muda mwingi wa kucheza winga akiwa na Mourinho na leo anacheza kati akiwa na Solskajaer na hivyo ana nafasi kubwa ya kufunga.

"Jambo jingine ambalo ni lazima niseme wakati Mourinho anaondoka Man United  alikuwa ana michezo mitano ambayo yote ilikuwa ni ya kushinda na kila ushindi unazidikukupa nguvu ndicho ambacho amekifanya Solskjaer kwa usahihi'' alisema Wenger

Hata hivyo amesema kwake yeye anaona Manchester United inawachezaji wazuri na vijana ambao wanaweza kufanya mashambulizi ya kushtukiza kama ambavyo anafanya Paul Pogba

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.