Header Ads

Wimbo wa tetema umewagusa wengi

Msanii wa muziki kutoka nchini Marekani, Kevin Gates ameonyesha kuukubali wimbo mpya wa
Rayvanny na Diamond Platnumz unaokwenda kwa jina la Tetema.

Mkali huyo aliyetamba na ngoma '2 Phones' ameweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akisikiliza wimbo huo akiwa kwenye gari lake.

Wimbo Tetema ulitoka wiki iliyopita na video yake ikatoka hapo juzi ambapo iliweza kufikisha watazamaji (views) Milioni 1 ndani ya saa 17 pekee kwenye mtandao wa YouTube na kuwa wimbo wa kwanza kwa Rayvanny kufanya hivyo.

Hata hivyo Rayvanny ameshindwa kuifikia rekodi ya Diamond kupitia wimbo wake 'Hallelujah'
aliowashirikisha Morgan Heritage ambao ulifikisha watazamaji Milioni 1 ndani ya saa 15 pekee

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.