Header Ads

40 wauwawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa baada ya kuzuka mashambulio katika misikiti miwili

Shambulio la kigaidi lauwa watu 40 New Zealand
Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern anasema watu 40 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya baada ya kuzuka mashambulio katika msikiti miwili katika mji wa Christchurch, huko New Zealand.

Waziri mkuu huyo amelitaja shambulio hilo kuwa mojawapo lililotanda 'kiza kikubwa' siku ya leo nchini humo.

Wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa, kamishna wa polisi Mike Bush anasema, lakini ameonya kwamba huenda washukiwa zaidi wapo.

Inaarifiwa kwamba washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa lakini ni wazi kwamba wana itikadi kali, Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.