Header Ads

Afungwa maisha kwa kumlawiti mtoto wa miaka minne


Mkazi wa Stakishari, Ombeni Said maarufu kwa jina la Nyoka (30) amehukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Ilala  baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Flora Haule amesema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka Mahakama imeopa pasi na shama mshtakiwa ametenda kosa hilo.

Pia  mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho alimtambua mshtakiwa huyo na ushahidi wa mama mzazi na daktari uliunga mkono hivyo kumuhukumu mshtakiwa huyo kutumikia kifungo cha maisha jela.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono aliiomba Mahakama itoe adhabu inayomstahili  kwa mshtakiwa huyo.

Kwa upande wake mshtakiwa alipopewa nafasi ajitetee kwa nini asipewe adhabu kali, aliomba asipewe adhabu kali kwa sababu anafamilia inayomtegemea.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 560 ya mwaka 2017,  Nyoka anadaiwa alitenda kosa hilo  kinyume cha kifungu cha 154(1)(a) na C cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Inadaiwa kuwa Oktoba 23, 2017 huko Stakishari wilaya ya Ilala Nyoka alimlawiti mtoto wa kike wa miaka nne

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.