Header Ads

Amber Lulu akiri kutumia mkorogo-Nikwambie kitu kila mtu anafanya kitu anachokipenda, mimi nimweusi lakini nilikuwa napenda kuwa mweupe


Mrembo kwenye kiwanda cha muziki wa kizazi kipya hapa nchini Ambar Lulu amekiri kutumia vipodozi maarufu kama Mkorogo ili kutengeneza muonekano wake.

Akizungumza kwenye kipidi cha The Playlist cha Times FM Amber Lulu amesema tangu zamani alikuwa anapenda kuwa mweupe kitu kilichopelekea kuamua kutumia gharama kubwa kutengeneza rangi hiyo.

"Nikwambie kitu kila mtu anafanya kitu anachokipenda, mimi nimweusi lakini nilikuwa napenda kuwa mweupe. So, nilifanya ninachokipenda pia unajua weupe sio kazi rahisi ni expensive (Gharama) natumia hela’’ amesema Amber Lulu

"Unaweza ukatumia mafuta alafu yasikupende, inabidi ubadirishe kwa mwezi naweza tumia mpaka million mbili’’ ameongeza Amber Lulu.

Kwa sasa Amber Lulu anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Makeke ambao amemshirikisha msanii Prezoo kutokea nchini Kenya.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.