Header Ads

auwawa na watu waliojichukulia sheria mkononi kata ya vihingo


Mtu mmoja ameuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi, kijiji cha Malale kata ya Vihingo, Mzenga Kisarawe mkoani Pwani kwa kufanya jaribio la kupora pikipiki huko Maneromango.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alisema, tukio hilo limetokea  usiku wa kuamkia march 15 mwaka huu na kumtaja aliyeuawa ni Omarry Abdallah maarufu Mboweto (50) mkazi wa Kagera ,Dar es salaam

Alieleza, marehemu kabla ya kuuawa akiwa na wenzake wawili wakitumia gari namba T. 613 DFG aina ya carrina walifika Maneromango na kufanya tukio hilo.

Watuhumiwa baada ya kuhojiwa wamekiri kujihusisha na matukio mawili ya uporaji tarehe 14 January mwaka huu huko Kitonga Kisarawe ambapo walipora pikipiki aina ya sanlg namba MC 324 CDL aina ya haoujue mali ya Haruna Goha.
Wankyo alisema, tukio jingine walilolifanya ni kupora bajaji eneo la Kibuta mali ya Shukuru Ally february 13 mwaka huu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.