Header Ads

Bodi ya utalii na kampuni ya Touchrod International Holdings Group yasaini makubaliano ya ushirikiano


DAR ES SALAAM:Bodi ya Utalii Tanzania na Kampuni ya Touchrod International Holdings Group imesaini makubaliano ya ushirikiano ambayo imepanga kuleta watalii 10,000 kutoka China katika kipindi cha mwaka 2019.

Hayo yameelezwa Jijin Dar es salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Jaji mstaafu Thomas Mihayo  wakati wakusaini makubaliano hayo ambapo amesema hatua kubwa iliyopigwa na sekta ya Utalii inaimarika na inakuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa nchi kupitia soko la Watalii kutoka nchini China.

Amesema kupitia taarifa za Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) na vyanzo vingine mbalimbali duniani kuwa soko la watalii kutoka China limeendelea kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watalii duniani na mchango katika uchumi wa dunia.Kwa upande wake Mkuu wa ujumbe huo kutoka china Mr Fu Wei amesema kampeni hiyo inahusisha nchi tatu za Afrika ambazo ni Tanzania,Zimbabwe pamoja na Djibout.

Hata hivyo Wadau wa sekta ya Utalii wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha jambo hilo muhimu kwa Taifa na kuhakikisha kuwa kila mmoja katika nafasi yake anatumia fursa ili kuleta maendeleo zaidi na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.