Header Ads

Bunge la Uingereza linataka zoezi la Brexit kucheleweshwa


Bunge la Uingereza linapendelea mpango wa kujitoa nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya-Brexit ucheleweshwe pamoja na kupigiwa kura kwa mara ya tatu mpango huo.

Wabunge mjini London wamepiga kura kwa sauti 413 dhidi ya 202 kuunga mkono mapendekezo yote mawili yaliyowasilishwa na serikali.

Waziri Mkuu Theresa May amesisitiza zoezi la Brexit litaweza kucheleweshwa kwa muda mfupi ikiwa wabunge watapiga kura kuunga mkono fikra hiyo machi 20 inayokuja-siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels.

Mkutano huo wa kilele utakaoanza Machi 21 utajadili uwezekano wa kucheleweshwa zoezi la Brexit hadi Juni 30 inayokuja. Pindi muda ukiwa mrefu zaidi, basi Uingereza italazimika kushiriki katika uchaguzi wa bunge la Ulaya.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.