Header Ads

China yajitolea kuisaidia venezuela


China imejitolea kuisaidia Venezuela kurejesha huduma za umeme, baada ya Rais Nicolas Maduro kumtuhumu mwenzake wa Marekani Donald Trump kwa kufanya kile alichokiita kuwa ni hujuma kwa kutumia udukuzi wa mtandaoni.

 Nchi hiyo ya Amerika Kusini inakabiliwa na hali mbaya zaidi ya kukatika umeme kuwahi kutokea nchini humo.

Maeneo mengi ya nchi hiyo hayajawa na umeme kwa siku sita mfululizo hali inayosababisha matatizo kwenye hospitali.

Akizungumza mjini Beijing, Waziri wa Mambo ya nchi za Kigeni wa China Lu Kang amesema kuwa China ina wasiwasi mkubwa kuhusu hali inayoendelea nchini Venezuela, isipokuwa hakutoa maeneo ya namna nchi hiyo inavyopanga kuisaidia Venezuela kurejesha huduma za umeme.

Maduro ambaye bado ana udhibiti wa jeshi na tasisi nyingine za serikali pamoja na kuungwa mkono na Urusi na China, anailaumu Marekani kusababisha mgogoro wa kiuchumi nchini mwake na akamkemea kiongozi wa upinzani Juan Guaido kwa kuwa kibaraka wa Marekani.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.