Header Ads

Dismas tena azungumzia kuhusu taarifa hii

Dismas Ten afunguka Ndemla kujiunga Yanga
Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten amezungumzia rasmi tetesi zinazosambaa kuhusu kiungo wa klabu ya Simba, Said Ndemla kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania bara.


Tetesi hizo zimeshika kasi baada ya Dismas Ten kupost picha ya Ndemla mara kadhaa hivi karibuni katika ukurasa wake wa Instagram huku akishiria kuwa kuna jambo kubwa liko njiani.

Mwenyewe amezunguzia sababu ya kuweka picha hizo na ukweli kuhusu Yanga kumsajili kiungo huyo wa mahasimu wao Simba, ambapo amesema, "Ndemla ni mchezaji mzuri na hakuna ambaye hafahamu juu ya uwezo wake. Ndemla mimi ni rafiki yangu na suala ya yeye kusajiliwa au kutosajiliwa Yanga linahusu benchi la ufundi na kamati yetu ya usajili".

"Yote yanaweza kusemwa mwisho wa msimu lakini kwa sasahivi huwezi kuzungumza lolote", ameongeza Ten.

Jana Machi 7, droo ya michuano ya shirikisho (ASFC) imepangwa na klabu ya Yanga imepangwa dhidi ya Alliance FC. Mechi zingine ni Kagera Sugar itapambana na Azam FC, KMC ikivaana na African Lyon huku Lipuli FC ikipangwa na Singida United.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.