Header Ads

Dkt Mahenge awahakikisha wakazi wa jiji la Dodoma jambo hili


DODOMA.Mkuu wa mkoa wa Dodoma dk binilith mahenge amewahakikishia wakazi wa jiji la Dodoma na wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini wanaohamia na kuwekeza Dodoma kuwa viwanja kwaajili ya makazi, biashara na uwekezaji vipo.

Ameyasema hayo akiwa kata ya mtumba wilaya ya Dodoma mkoani hapa katika ziara yake ya kikazi ambapo amewapongeza mkurugenzi wa jiji la Dodoma mstahiki meya na mkuu wa wilaya ya Dodoma kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kupima viwanja akisema awali kasi ya uhitaji wa viwanja ilikuwa kubwa kuliko kasi ya upimaji lakini hivi sasa kasi ya uhitaji ni ndogo kuliko kasi ya upimaji. .

Aidha amesema maeneo yote aliyopita katika ziara hiyo miundombinu ya barabra ipo hivyo changamoto kubwa wanayotakiwa kuiangalia kwa upimaji wa baadaye ni miundombinu ya maji na umeme.

Katika kuufanya mji kuonekana kama makao makuu ya nchi dk mahenge amesema maeneo yaliyopimwa yasimamiwe vizuri ili kusitokee ujenzi holela.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma patrobas katambi amemshukuru mkuu wa mkoa kwa kufanya ziara hiyo.


Naye mkurugenzi wa jiji la Dodoma godwin kunambi amesema katika eneo hilo kuna takriban viwanja elfu 10 na upande wa kuna viwanja elfu 5 vya lamaa akisema jiji la Dodoma halifanyi kazi lenyewe bali linahusisha sekta binafsi katika kupanga jiji la Dodoma.


Hata hivyo kunambi amesema wako tayari kutekeleza maelekezo ya mkuu wa mkoa na kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kufanya kazi kwa pamoja.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.